Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ngoma ya Kimombo ya Zuchu yazua jambo mitandaoni

ZUCHU NGOZI Ngoma ya Kimombo ya Zuchu yazua jambo mitandaoni

Fri, 28 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwimbaji wa nyimbo za bongofleva nchini Tanzania Zuhura Othman Soud maarufu Zuchu ameachilia wimbo uliojawa na ung’eng’e ambao umezua ngumzo na kuibua hisia mseto katika mitandao ya kijamii.

Zuchu alimshirikisha Nana Fofie katika wimbo wa Kiingereza unaojulikana kama Seasons (TEASER) ambao umepatwa kutazamwa YouTube na watazamaji elfu 28 chini ya saa 12 ambapo kumekuwa na ngumzo juu ya ukali wake.

Katika mtandao wake wa Instagram, msanii huyo aliposti wimbo huo ambapo alisema kuwa hicho ni kionjo tu mengine zaidi yaja na hivyo mashabiki wake wasichoke kusubiri kwa kuwa anawaandalia mengi.

Baadhi ya wanamitandao wanazidi kumtania kwa wimbo huo, kwani wengi wanadai kuwa hawakufahamu kuwa mpenzi huyo wa Diamond Platnumz anakimanya Kimombo kama kinavyojitokeza katika wimbo wake.

“Kwanzia leo chuchu unakiti chako pepopi sasa ulikuwa wapi siku zote wanakufananisha fananisha ni mimi shabiki wa mziki mzuri tuu,” mmoja alimtania.

Wengine pia waliendelea kumpongeza kwa kipaji chake cha kipekee katika muziki ambapo walidai kuwa wimbo huo utakuwa miongoni mwa nyimbo kali sana bara la Afrika na hivyo azidi kusonga mbele.

“Mwanadada unachokipaji na talanta unayo, wewe ni shujaa na zaidi ya shujaa wa kike katika usanii, tunakupenda sana nchini Nigeria zidi kunawiri na kushamiri,” Mwingine alitoa hisia zake.

Haya yanajiri wakati ambapo mwanamuziki wa nyimbo za sekula nchini Kenya aliwarai wasanii kuanza nchini Kenya na Afrika Mashiriki kuanza kuimba za kimombo aghalabu ili ziweze kuafikia malengo ya kimataifa kwani zinawafanya kuwa maarufu zaidi ikilinganishwa na wanazoimba za Kiswahili.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live