Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ngoma nayoisikiliza ni ‘Seduce Me’, sio ya kishamba – Bibi Cheka

Wed, 7 Feb 2018 Chanzo: bongo5.com

Bila shaka unamkumbuka Bibi Cheka aliyefanya vizuri na ngoma ‘Ni Wewe’ aliyoshirikiana na Mh. Temba katika ‘kundi’ la Mkubwa na Wanawe.



Bibi Cheka katika mahojiano na Planet Bongo ya EA Radio amesema katika kipindi hiki ambacho amekuwa kimya ngoma ya Bongo Flava ambayo imemvutia zaidi ni Seduce Me ya Alikiba.

“Ngoma nayoisikiliza naipenda ni ya Alikiba (Seduce Me), imeingia ya kimjini mjini sio ya kishamba, ile ilitoka halafu siku ya pili inatoka ya Diamond, naikubali sana,” amesema.

Katika hatua nyingine amesema ukimya wake umeshababishwa na kuugua lakini hakupata msaada wowote kutoka kwa watu aliokuwa akifanya nao kazi ndani ya Mkubwa na Wanawe.

Chanzo: bongo5.com