Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Neymar akacha tuzo aponda raha Rihanna

58677 Neymar+pic

Mon, 20 May 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Paris, Ufaransa. Neymar amekacha sherehe za kupokea tuzo ya mwanasoka bora wa mwaka wa Ufaransa na kwenda kuponda raha na mwanamuziki, Rihanna katika klabu za usiku.

Neymar ameonyesha jinsi anavyoweza kufanya kazi kwa bidi na kucheza kwa nguvu wakati alipokuwa katika klabu ya usiku na Rihanna. 

Nyota huyo wa PSG wenye thamani ya pauni 198 milioni baada ya kuugua kwa muda mrefu, alitumia muda wake usiku wa jana kupiga picha na mwanamuziki huyo wa Marekani.

Picha hiyo katika ukurasa wake wa Instagram akiwa ameweka kidole mdomoni huku akiwa karibu na Rihanna imeweza kuwavitia followers 187m. 

Nyota huyo wa Brazil alindika ujumbe: 'Queen and powerful woman.'

Neymar hakuwepo katika sherehe za kutoa tuzo ya mchezaji bora wa mwaka Union Nationale des Footballeurs Professionnels (UNFP) iliyofanyika jana usiku huku nyota mwenzake wa PSG, Kylian Mbappe akitwaa tuzo mbili.

Pia Soma

Mbappe mwenye miaka 20, alikuwa na msimu mzuri katika Ligue 1 akiwa kinara wa mabao 30.

Mbappe alishinda tuzo ya mchezaji bora wa mwaka wa Ligue 1 na mchezaji bora chipukizi wa mwaka huku Neymar, pamoja na kuwa majeruhi alifanikiwa kuingia katika kikosi bora cha mwaka.

Neymar na PSG alitawala katika timu ya mwaka ikiwa na wachezaji sita katika kikosi hicho: Marquinhos, Thiago Silva, Angel Di Maria, Marco Verratti, Neymar na Mbappe.

Chanzo: mwananchi.co.tz