Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Neema yawadondokea Ray, JB

Ray3 Mwigizaji Ray

Sat, 19 Feb 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

WAANDAAJI wa filamu Afrika Mashariki hususan waandishi wa miswada (script writters) watanufaika na mpango maalum ulioandaliwa na Taasisi ya Realness kwa ajili ya kuwapa mafunzo waandaaji wa filamu kutoka barani Afrika.

Watayarishaji kama kina Ray, JB na wengine watapata neema ya kusafiri na kwenda kujifunza zaidi katika nchi za Nigeria, Afrika Kusini na Uswisi.

Waandaaji hao wa filamu kutoka Afrika Mashariki, watashindanishwa ambapo watakaoingia nafasi ya Sita Bora, ndiyo watakaopata nafasi ya kushiriki kwenye mafunzo yatakayofanyika katika nchi hizo tatu katika awamu ya saba ya mafunzo hayo yatakayoanza Agosti 3 hadi Novemba 13, 2022.

Habari njema katika mafunzo ya mwaka huu, ni kwamba Taasisi ya Realness inashirikiana na na Chuo cha Locarno Filmmakers’ Academy cha nchini Uswisi na kuwapa fursa wote watakaokidhi vigezo, kwenda kushiriki katika maonesho ya filamu ya Locarno Film Festival pamoja na kuhudhuria mafunzo maalum yanayoendeshwa na chuo hicho maarufu kama BaseCamp.

Watu sita wenye bahati watakaokidhi vigezo, watakaa kwa muda wa wiki sita katika vituo vya kukuza vipaji vya Nirox na Farmhouse 58 vilivyopo nchini Afrika Kusini na kupata nafasi ya kunolewa na wakufunzi waliobobea; Selina Ukwuoma, Mmabatho Kau na Cait Pansegrouw.

Baada ya kumaliza mafunzo, Mkurugenzi wa Taasisi ya Realness, Elias Ribeiro atasafiri na washiriki hao mpaka nchini Uswisi katika Tamasha la Locarno Film Festival huku Mehret Mandefro ambaye ni Mkurugenzi wa Maendeleo wa Realness, ataongozana na washiriki hao mpaka Nigeria kushiriki maonesho ya kimataifa ya filamu ya Africa International Film Festival (AFRIFF).

Chanzo: www.tanzaniaweb.live