Lifestyle

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

SIL

Ndoa yavunjika, Bibi harusi adakwa na Polisi

Skynews Bride Arrest Mexico 6423119 Ndoa yavunjika, Bibi harusi adakwa na Polisi

Wed, 17 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Bibi harusi kutoka nchini#Mexico aitwaye Nancy N amekamatwa na polisi siku ya harusi yake kwa tuhuma za unyang’anyi.

#NancyN alikamatwa wakati alipokuwa akishuka kwenye gari akiwa anaelekea kanisani huku mumewe mtarajiwa aitwaye #ClementN, akifanikiwa kutoroka.

Kwa mujibu wa vyombo vya habari nchini humo vimeripoti kuwa wawili hao na wengine sita wanatuhumiwa kwa kufanya unyang’anyi kwa wafanyabiashara wa kuku mji mkuu wa #Mexico.

Watuhumiwa hao wanadaiwa kuwateka wafanyabiashara wa maduka ya kuku na kuchukua kuku kisha kuwafungia katika ghala. Ofisi ya mwendesha mashtaka imeweka wazi kuwa uchunguzi bado unaendelea.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live