Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

"Ndoa yangu nitaifanya kwenye meli" - Mkojani

MK "Ndoa yangu nitaifanya kwenye meli" - Mkojani

Mon, 12 Apr 2021 Chanzo: eatv.tv

Mchekeshaji maarufu kwa sasa nchini Tanzania Mkojani Mpango amesema anataka harusi yake iwe ya kitajiri na ataifanya baharini ndani ya meli ifikapo mwezi wa 7 mwaka huu.

Submitted by Shaluwa Anta on Jumatatu , 12th Apr , 2021 Mchekeshaji Mkojani

Mkojani amesema ndoa yake ilipangwa kufanyika mwezi wa 3 mwaka huu lakini kutokana na mipango na sababu za kifamilia ikashindikana kufanyika, na lengo la kufanya harusi yake kwenye meli ni kutaka iwe na ukubwa wa aina yake.

"Nina mipango ya kuoa, ndoa yangu ilikuwa ifanyike mwezi wa 3 lakini sababu za kifamilia ikashindikana, harusi yangu nataka niifanye kwa ukubwa fulani iwe ndani ya meli na ya kitajiri, nadhani mwezi wa 6 au 7 itakuwa tumeshakamilisha hilo jambo, mchumba wangu tayari naishi nae na nimeshatoa barua" amesema MkojaniĀ 

Zaidi mtazame hapa chini kwenye video.

Chanzo: eatv.tv