Katika hali ya sintofahamu kuhusiana na ndoa ya #Manara na mkewe #RushayNah, inaelezwa kuwa ipo matatani baada ya wawili hao kufuta urafiki wao katika kurasa zao za #Instagram.
Huku mrembo #RushayNah ambae alifunga ndoa na #Manara mwaka jana na kuwa mke mdogo kushindwa kuzuia hisia zake kwa kuja juu na kutaka video yake ifutwe katika kurasa moja ya #Instagram iliyokuwa inayoonesha #Manara na #RushayNah wakicheza muziki iliyosindikizwa kwa ujumbe usemao “Bugati na Pisi yake”.
Akihojiwa na Soud Brown wa Clouds FM kuhusu kuvunjika kwa ndoa hiyo, Manara amemtolea povu mtangazaji huyo huku akimtukana matusi makali na kumwambia sio kazi yake kufuatilia maisha ya ndoa za watu.
Inadaiwa kuwa, tayari Rushay Nah tayari ameshaondoka Dubai alikokuwa na mumewe huyo na ameshatua nchini Tanzania.