Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ndoa ya Davido na Chioma kusimamisha Afrika leo

Davido Na Chioma Ndoa.jpeg Ndoa ya Davido na Chioma kusimamisha Afrika leo

Tue, 25 Jun 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Hivi majuzi zilisambaa picha mfululizo za kuvutia za wapenzi wa kitambo wa Nigeria na mastaa wakubwa barani Afrika, Davido na Chioma.

Picha hizo za kabla ya ndoa zimezua mhemko kwenye mitandao ya kijamii, zikidokeza ukubwa na ufalme utavyokuwa katika harusi yao ya kitamaduni iliyotarajiwa kufungwa Jumanne ya Juni 25, 2024 katika Hoteli ya kifahari ya Eko huko Lagos nchini Nigeria.

Picha hizo, ziliachiwa kwenye akaunti ya Instagram ya staa huyo mkubwa wa muziki barani Afrika aliyewahi kutajwa kwenye Tuzo za Grammy mara moja. Picha hizo zimevuta hisia za mashabiki wa wapenzi hao hivyo kusababisha shauku ya kuona tukio hilo.

Wakiwa kwenye mavazi ya kitamaduni ya kuvutia, Davido na Chioma wanaonesha haiba na mabaha mazito, wakithibitisha kwamba harusi yao hiyo itasimamisha ulimwengu wa burudani Afrika na kwingineko duniani.

Katika mojawapo ya picha hizo, Davido amevalia agbada iliyotengenezwa kwa kitambaa cha aso oke chenye rangi nyingi, kilichopambwa kwa darizi za manjano kwa umaridadi huku Chioma aking’aa kwa gauni refu jeusi, lililopambwa kwa skafu ya kitambaa kimoja kilichofungwa saizi yake.

Picha nyingine iliangazia mandhari ya rangi ya dhahabu na njano huku Davido akiwa ameketi kwenye kiti cha kifalme, akiwa ameshikilia fimbo yake na huku Chioma akisimama upande wake wa kulia na fimbo ya Kiafrika mkononi.

Seti tatu ya picha iliangazia Davido na Chioma wakiwa wamevalia mavazi meusi na mandhari nzuri iliyopambwa kwa vivuli tofauti vya manjano.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live