Lifestyle

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

SIL

Ndoa nyingi zinavunjika sababu ya kipato - Baba Levo

Mwanamke Hatongozwi, Anaalikwa Tu Baba Levo.png Ndoa nyingi zinavunjika sababu ya kipato - Baba Levo

Wed, 15 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Msanii wa Tanzania, Revokatus Kipando, almaarufu Baba Levo, kupitia kituo kimoja cha Radio amefunguka kuhusu ndoa huku akisema kuwa nyingi yazo huvunjika mwanamke anapopata ajira.

Kulingana na Baba Levo wanawake wengi kwenye ndoa wakipata hela zao hudharau ndoa kwa misingi kwamba wanaweza kujikimu.

"Asilimia kubwa ya kuvunjika kwa ndoa nyingi zinachangiwa na wanawake, wanapota fursa ya kujifanyia kazi wanapopata hela zao wengi huanza kuwadharau wanaume wao kwa kuwa wanaweza kujigharamia kimaisha,"alisema.

Msanii huyu alidokeza kwamba kulingana na tamaduni zilizotumika miaka ya nyuma wanawake hawangeruhusiwa kufanya kazi ,jukumu la kufunya kazi ilikuwa la wanaume, jambo ambalo kwa sasa limezikwa kwenye kaburi la sahau.

"Ndoa za kitambo zilidumu kwa kuwa mila zingefuatwa ila kwa sasa kuna mashirika yamejitokeza kutetea haki za wanawake ndio chanzo cha wana wanawake kupata fursa ya ajira jambo ambalo limechangia talaka,"alisema.

Baba Levo kwenye kauli yake aliongeza kuwa wanawake wengi hawajazoea kujifanyia ajira ila kwa wakati wanapopata ajira wengi zile hela wanazopata huwachanganya zaidi.

"Wanawake wakipata hela wanachanganywa nazo huku wengi wakitaka kuishi maisha yao wenyenye bila usubufu wotote,"alisema Baba Levo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live