Lifestyle

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

SIL

Ndoa iliyodumu miaka 24 yavunjika Mume kabaini watoto watatu sio wake

72847 NDOA+PIC Ndoa iliyodumu miaka 24 yavunjika Mume kabaini watoto watatu sio wake

Tue, 5 Jan 2021 Chanzo: millardayo.com

Hebu fikiria, mmeishi kwenye ndoa kwa miaka 24, baadae unagundua kuwa watoto watatu kati ya wanne ambao umekuwa ukiwalea pamoja na mke wako si wako.

Katika tukio hilo lililotokea nchini Kenya, shuhuda ambaye ni rafiki wa karibu wa bwana huyo, Julius Mmasi amefichua kuwa rafiki yake huyo wa karibu amelazimika kuvunja ndoa hiyo iliyodumu kwa miaka 24.

Hatua hiyo imekuja baada ya matokeo ya DNA kubainisha kuwa ni baba halisi wa mtoto mmoja pekee kati ya wanne ambao aliwalea pamoja na mke wake.

Jambo la kuhuzunisha zaidi ni kuwa mke wake amekiri kuwa bosi wake ndiye baba ya watoto watatu wa kwanza.

Kwa mujibu wa Mmasi, rafiki yake huyo aliamua kufanyia watoto wake wanne uchunguzi wa DNA baada ya kuanza kumshuku mke wake.

Baada ya uchunguzi huo aligundua kuwa mabinti wake watatu ni watoto wa bosi wa mke wake huku kitinda mimba ambaye ni wa kiume ndiye mtoto wake pekee halisi katika ndoa hiyo.

“Watoto watatu wa kwanza wa kike, wawili walifuzu mwingine yuko kidato cha nne. Mke wake alikiri kuwa watoto watatu wa kwanza ni wa bosi wake. Utamshauri mtu kama huyu vipi kuhusu haya?, ndoa ya miaka 24 imevunjika ghafla, maana kuwa wanaume wengi wakiamua kuchukua hatua hii ndoa nyingi zitavunjika” Mmasi.

HOTEL YA SUGU KUBOMOLEWA, RAIS MAGUFULI AZUIA “MSIBOMOE HOTEL SUGU, MSILETE SIASA”

Chanzo: millardayo.com