Lifestyle

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

SIL

Ndoa Yavunjwa kwa Talaka ya Tsh Tril 1.4

PrincessSheikhDivorce 1 Sheikh Mohammed Al Maktoum na mkewe

Tue, 21 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wakati watu wakiendelea kufunga ndoa za gharama, pia kuna ndoa ambazo zinaendelea kuvunjika kwa gharama kubwa. Huko nchini Uingereza aliyekuwa mke wa zamani wa mtawala wa Dubai, Princess Haya bint Hussein ametunukiwa na mahakama kuu nchini humo Pauni Milioni 554 (sawa na trilioni 1.4 Tsh) kama fidia ya talaka aliyopewa na mume wake Sheikh Mohammed Al Maktoum.

Fidia hiyo ya talaka imetajwa kuweka rekodi ya kuwa ni fidia kubwa zaidi kuwahi kutokea nchini Uingereza, ambapo Pauni Milioni £251 itatumika kwa gharama za usalama ili kumlinda binti wa kifalme “Princess Haya na watoto wake wawili dhidi ya kutekwa nyara, na Pauni milioni 290 zitatumika kwa ajili ya matunzo ya watoto hao kwa maisha yao yote.

Chanzo cha ndoa hiyo kuvinjika kinatajwa kuwa ni baada ya Princess Haya kugundulika kuwa na uhusiano wa kimapenzi na bodyguard wake.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live