Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ndege ya Diamond ipo njiani-Baba Levo

Ndege Ya Diamond Ndege ya Diamond ipo njiani-Baba Levo

Mon, 28 Nov 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Chawa wa WCB, Baba Levo ameeleza kuwa, suala la ndege mpya aliyonunua Diamond kutua nchini ni suala la muda tu.

Baba Levo ametoa kauli hiyo mara baada ya kubanywa na waandishi kuhusu baadhi ya madai kuwa, Diamond hajanunua ndege hiyo kama ambavyo baadhi ya wadau akiwemo Carrymastory amesema.

"Carrymastory ni mwehu tu kama wehu wengine, asituletee hizo. Ndege sio kama Bajaj unaagiza leo na kuja leo. Ndege tumeshalipia, itakuja. Kuna mambo mengi ya kukamilisha hadi ndege itue ikiwemo taratibu za kiserekali," alisema Baba Levo.

Mapema mwaka huu, meneja wa Diamond, Salam alisema wameamua kununua ndege hiyo kutokana na kupoteza gharama nyingi kwenye kusafiri nchi mbalimbali kwa kulipia tiketi za ndege hivyo bora wanunue ndege yao ambayo pia watakuwa wanaikodisha.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live