Sonona (depression) ni ugonjwa wa afya ya akili ambao unaweza kuathiri jinsi watu wanavyofikiri, kuhisi, na kutenda, na huathiri takribani watu milioni 350 duniani kote.
Takwimu za Shirika la Afya Duniani (WHO) zinaonesha kuwa sonona ndio chanzo kikuu cha ulemavu duniani, huku zaidi ya watu milioni 264 wakiwa na msongo wa mawazo wa wastani hadi hatua mbaya zaidi.
Utafiti unaonesha kuwa wanawake wana uwezekano mara mbili wa kukumbwa na mfadhaiko ikilinganishwa na wanaume, na nchi za kipato cha chini huwa na viwango vya juu vya sonona kuliko nchi zenye mapato ya juu.
Zaidi ya hayo, takwimu za WHO zinaonesha kuwa matatizo ya mfadhaiko kwa vijana yamekuwa yakiongezeka katika muongo mmoja uliopita, na zaidi ya watu 800,000 hufa kutokana na kujiua kwa sababu ya mfadhaiko kila mwaka.
Hizi ni orodha ya nchi 10 ambazo watu wake wanaongoza kupata sonona duniani;
1. Greece – 6.52%
2. Spain – 6.04%
3. Portugal – 5.88%
4. Palestine – 5.75%
5. Tunisia – 5.75%
6. Bahrain – 5.52%
7. Morocco – 5.49
8. Iran – 5.48%
9. Lithuania – 5.42%
10. Ukraine – 5.25%.