Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nay wa Mitego atuhumiwa kwa uchochezi

Nay 9 WA0007 Nay wa Mitego.

Wed, 6 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baada ya taarifa kusambaa zikimhusisha Msanii nguli wa Hip Hop Bongo, Emmanuel Elibariki maarufu kama 'Nay wa Mitego' kufunguliwa madai ya Uchochezi, Wakili wake, Jebra Kambole amethibitisha hilo.

Kambole amesema kuwa Mteja wake alipata wito wa Jeshi la Polisi Kituo cha Kati-Dar kwa tuhuma za uchochezi kupitia baadhi ya mashairi ya wimbo wake wa 'Amkeni'.

Kuhusu madai ya Nay wa Mitego kuzuiwa na #BASATA kufanya matamasha, Jebra amesema hakuna taarifa rasmi kutoka BASATA, japokuwa BASATA walikuwa wakiwasiliana na Maofisa Utamaduni wa Mikoa ambao ndio walimnyima Mteja wake vibali.

Pia, Jebra amesema BASATA imempa Nay wa Mitego wito wa kwenda Ofisini kwao bila Mwanasheria Septemba 8, 2023.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live