Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nay wa Mitego ajuta "Sitaki kujionesha tena"

N Nay wa Mitego ajuta "Sitaki kujionesha tena"

Tue, 6 Jul 2021 Chanzo: eatv.tv

Nay wa Mitego amesema amejifunza mambo mengi hivyo hataki kuyaonyesha maisha yake kwenye mitandao ya kijamii kama ilivyokuwa mwanzo akifanya 'show off' za mali zake kama gari, nyumba  au hata mpenzi wake.

Msanii huyo amesema hivyo kwa sababu anaamini mashabiki wake wengi ni wale wa hali ya chini na wa mtaani hivyo hataki kuwaumiza roho kwani bado anahitaji sapoti yao kwenye shughuli zake za kimuziki.

"Sitaki kujionyesha tena watu wanajua kama nafanya muziki sipendi ku-show off, watu wanaonisapoti kula yao ni shida lakini wananipenda, mashabiki wangu wengi asilimia kubwa ni walala hoi, watafutaji, wamachinga wanamaisha ya kuungaunga sitaki kuwaumiza roho bado nahitaji sapoti yao" ameeleza Nay wa Mitego 

Zaidi mtazame hapa chini akizungumzia suala hilo.  

Chanzo: eatv.tv