Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nay wa Mitego adai ngoma ya Diamond ‘Iyena’ hata angeitupa barabarani inge-hit

8576 NAYWA TZW

Mon, 4 Jun 2018 Chanzo: bongo5.com

Rapper Nay wa Mitego ametoa neno katika ngoma mpya ya Diamond Platnumz ya ‘Iyena’ amesema hata angetupa ngoma hiyo barabarani inge – hit tu.



Nay amesema kuwa licha ya kwamba ngoma kali yupo na mzazi mwenzie mwenye nyota na mafanikio, Zari The Bass Lady, amemtaka msanii huyo kuendelee kupuyanga na wachafua nyota.

“Mzee Mwenzangu Diamond platnumz Hii Ngoma Iyena Ata Ungeenda Kuacha Tu Barabarani Ukajifanya Kama Umeitupa Inge Hit Tu. Licha Ya Kwamba Ngoma Kali Pia Upo Na Mkeo Original Mama Tee Mwenye Nyota Ya Hela Na Mafanikio. Sasa Wewe Endelea Kupuyanga Na Hao Mapugi Machafua Nyota. Nitaongea Na Mama Tee Yaishe Tu.(Yamoyoni) Haya Fanya Muende YouTube,” ameandika Nay wa Mitego kupitia mtandao wake wa Instagram.

Hata hivyo utakumbuka miaka mitano iliyopita Diamond na Nay wa Mtego walitoa hit iliyokwenda jina la Muziki gani, hata hivyo hawakuishia hapo baadaye walitoa ngoma nyingine inaitwa ‘Mapenzi Pesa’.

Loading...
Chanzo: bongo5.com