Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nay wa Mitego: Walioko madarakani wanaogopa nyimbo zangu

Nay Wa Mitego Army Nay wa Mitego: Walioko madarakani wanaogopa nyimbo zangu

Mon, 9 Oct 2023 Chanzo: BBC Swahili

Mashabiki wake hupenda kumuita 'Rais wa Kitaa', Emmanuel Elibariki, maarufu Nay wa Mitego ni miongoni mwa wasanii wa muziki nchini Tanzania ambaye tungo zake mara kadhaa zimemtia matatani kutokana na mamlaka za udhibiti wa maudhui kutoridhishwa na tungo zake.

Akizungumza na BBC Swahili, Nay amesema viongozi walioko madarakani wanaogopa nyimbo zake ndiyo maana kutwa kucha amekuwa akiitwa BASATA, Polisi na kwenye mamlaka nyingine ili kujaribu kumnyamazisha huku yeye akidai kuwa yupo tayari kwa lolote lakini hatonyamaza.

"Sipendi siasa kwa sababu kwa sasa uwanja wangu ni mpana kuliko mwanasiasa ndiyo maana hata walioko kwenye mamlaka wanaogopa nyimbo zangu. Mimi nazungumza kama msanii, nikiwa kwenye siasa nitazungumza kama mwanasiasa.

"Kuna watu watakuwa hawapendi labda chama changu (CHADEMA) ambacho ni nipo kwa sababu wanaamini katika chama chao walichopo, kwa hiyo hata kama nikiongea kitu sahihi kuna wataki ataamua tu asinielewe kwa sababu mimi sio mtu wa chama chake.

"Nimeamua kufanya aina hii ya muziki kwa sababu kuna vitu ninaona vinatakiwa visemwe, hali imekuwa mbaya, vitu vinachukuliwa poa na hakuna wa kusema. Wakati mwingine viongozi hawana watu sahihi wa kuwaambia ukweli. Wengine wanaona wakisema ukweli kesho watakuwa hawana kazi, acha mimi niwasaidie," amesema Nay.

Chanzo: BBC Swahili