Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nay wa Mitego: Wakati wa magufuli nilifunguliwa kesi

Nay Wa Mitego Sauti Ya Watu VD Nay wa Mitego.

Mon, 9 Oct 2023 Chanzo: BBC Swahili

Mashabiki wake hupenda kumuita 'Rais wa Kitaa', Emmanuel Elibariki, maarufu Nay wa Mitego ni miongoni mwa wasanii wa muziki nchini Tanzania ambaye tungo zake mara kadhaa zimemtia matatani kutokana na mamlaka za udhibiti wa maudhui kutoridhishwa na tungo zake.

Akizungumza na BBC Swahili, Nay amesema viongozi walioko madarakani wanaogopa nyimbo zake ndiyo maana kutwa kucha amekuwa akiitwa BASATA, Polisi na kwenye mamlaka nyingine ili kujaribu kumnyamazisha huku yeye akidai kuwa yupo tayari kwa lolote lakini hatonyamaza.

"Kipindi nimetoa wimbo wa 'ALISEMA' nilipitia changamoto kubwa sana, ilikuwa kipindi cha Hayati JPM (aliyekuwa Rais wa tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli), kuna wakati walikuwa hawataki vitu viende kwenye medai. Nilikuwa naitwa polisi na BASATA. Nikienda BASATA nakutana na polisi ndani.

"Ikafika wakati nikaambiwa ukitaka kuachia wimbo inabidi upitie kwa kiongozi flani, nae ataupeleka sehemu flani kisha utaruhusiwa kuutoa. Nilifunguliwa pia kesi Kituo Kituo Kikuu cha Polisi (Sentro) nilikuwa nakwenda kuripoti kila baada ya siku tatu au nne," amesema Nay.

Chanzo: BBC Swahili