Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nay wa Mitego: Siwalaumu Media kutocheza nyimbo zangu - VIDEO

Nay Wa Mitego 2 Nay wa Mitego: Siwalaumu Media kutocheza nyimbo zangu

Wed, 16 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais wa Kitaa, Emmanuel Elibariki 'Nay wa Mitego amesema, halaumu chombo chochote cha habari (media) kutocheza nyimbo zake kwani nao wanalinda 'ugali' wao.

Nay amesema, anamshukuru Mungu ameshajitengenezea kundi kubwa la mashabiki hivyo hata wimbo wake usipochezwa kwenye media, bado unakwenda trending kwa kusikilizwa au kutazamwa na watu wengi.

"Mimi hata nikitoa wimbo wangu nikaenda kuutupa pale Manzese au Kariakoo, utasambaa tu Tanzania nzima hivyo sina sababu ya kuwalaumu media," alisema Nay.

Miongoni mwa ngoma za Nay ambazo hazichezwi kwenye media ni pamoja na Amkeni ambao ameutoa hivi karibuni.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live