Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nay wa Mitego: Nimenyimwa vibali vya shoo

Nay Wa Mitego Na Diamond Wakifanya Yao Nay wa Mitego: Nimenyimwa vibali vya shoo

Mon, 9 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mashabiki wake hupenda kumuita 'Rais wa Kitaa', Emmanuel Elibariki, maarufu Nay wa Mitego ni miongoni mwa wasanii wa muziki nchini Tanzania ambaye tungo zake mara kadhaa zimemtia matatani kutokana na mamlaka za udhibiti wa maudhui kutoridhishwa na tungo zake.

Akizungumza na BBC Swahili, Nay amesema viongozi walioko madarakani wanaogopa nyimbo zake ndiyo maana kutwa kucha amekuwa akiitwa BASATA, Polisi na kwenye mamlaka nyingine ili kujaribu kumnyamazisha huku yeye akidai kuwa yupo tayari kwa lolote lakini hatonyamaza.

"Familia yangu haiko tayari kwa sababu hiki sio kitu chao, hiki ni kitu changu, ndio maana hata nilipoanza kuimba muziki wao hawakuwa tayari wala hakuna mtu aliyenisapoti.

"Kwa hiyo kinawatesa zaidi wao kuliko mimi ambaye ninakamatwa na polisi, ninaitwa BASATA, nimefungiwa kufanya shoo, changamoto ni nyingi. Sipewi vibali vya shoo, ninazuiliwa kufanya shoo lakini mimi nipo tayari, huwa napokea kila kinachokuja kwa sababu najua hii sio kazi rahisi.

"Wimbo wangu mimi usipo-hit mtandaoni sichanganyikiwi kabisa na siwazi, zmiki wangu nisipousikia mtaani nachanganyikiwa. Mashabiki wangu wengi ni wale ambao kupata buku mtaani ni kazi kubwa, hawa kwa wiki wanaingia mtandaoni mara moja tu, ili mziki wangu umfikie lazima mimi huku chini niusukume," amesema Nay.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live