Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nay na Nini mahaba yamewazidia

Nay Na Nini Nay na Nini mahaba yamewazidia

Wed, 2 Mar 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rapa mtata Bongo, Nay Wa Mitego mara kadhaa amekuwa akihusishwa kutoka kimapenzi na msanii wake aitwaye Nini huku akikanusha.

Kwa upande wake, Nini ambaye yupo kwenye Lebo ya Nay Wa Mitego ya Free Nation amekuwa akikazia tu kuwa wao ni marafiki na wanafanya kazi tu.

Hata hivyo, kwa sasa inaonekana mahaba yamemzidia Nay na kuamua kutokuficha tena. Kupitia ukurasa wake wa Insta, Nay amemtakia heri ya kuzaliwa mrembo huyo ambaye anasheherekea siku ya mfanano wa kuzaliwa huku ujumbe aliomuandikia ndiyo uliozua mjadala mzito;

Nay amemuandikia Nini; “Leo kazaliwa mshkaji wangu, kipenzi changu, partner wangu, mchizi wangu Kabisaaa @niniofficialtz Happy Birthday to you Mama Chanja wangu. Mungu akupe maisha marefu zaidi. Enjoy your day Madame…”

Kwa upande wake, Nini amemjibu Nay; “Baba Chanja wangu…Thank u partner…” Wengi wamekuwa wakijiuliza hilo jina la Mama Chanja lina maana gani?

Chanzo: www.tanzaniaweb.live