Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nay Wa Mitego ataja sababu za Roma kukimbia TZ

Ney Ney Nay Wa Mitego ataja sababu za Roma kukimbia TZ

Sun, 21 Jun 2020 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kupitia mtandao wa Instagram Nay Wa Mitego amemchana Roma Mkatoliki baada ku-comment kwenye wimbo wake wa Mungu Yuko Wapi, kwenye post hiyo Nay amesema Roma anajitoa ufahamu, ametaja sababu za Roma kukumbia Tanzania, pia amemshauri arejee kwani kuwa watu wanaweza kutembea na mke wake.

"Mpendwa Roma Mkatoliki wewe ni mshkaji wangu ila kuna wakati nadhani unajitoa ufahamu sijui, kwamba wewe unaimba nyimbo ambazo Bi mkubwa akisikia wala hawezi kupanic wala kupanikishwa na watu baada ya wimbo kuzua mijadala, kwanza umekimbia nchini kwa sababu ya wimbo wa "Naitwa Roma".

"Kipindi ulivyotekwa mimi binafsi sikulala siku mbili tulikua tunashinda polisi Osterbay, Mama Roma alisema hataki tena uimbe muziki, ukiwa unanishauri muda mwingine usijifanye wewe ni mlokole kama unaimba Gospel, kuhusu huu wimbo wa Mungu yuko wapi wala hukutakiwa kutia neno coz wewe ni mwana sana"

"Nikushauri tu mwanangu fanya urudi watu watapita na mkeo, hakuna mwanamke anayeweza kuvumilia kukaa mwaka mzima bila ya kujamiiana, hao wanawake walishakufaga enzi za mababu zetu, kama una mpenda mkeo na watoto fanya urudi hakuna mtu wakukukamata mambo ya wimbo yalishapita" ameandika Nay Wa Mitego

Chanzo: www.tanzaniaweb.live