Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Navy Kenzo ni kazi juu ya kazi tangu 2008

Navy Kenzo 1234.jpeg Navy Kenzo ni kazi juu ya kazi tangu 2008

Wed, 5 Jun 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kundi la Navy Kenzo linaloundwa na Nahreel na Aika lilianzishwa mwaka 2013 ingawa walikuwa pamoja kimuziki tangu 2008 walipokuwa wanasoma nchini India.

Navy Kenzo ni jina ambalo limekutanisha maneno mawili kutoka nchi mbili tofauti, kwanza ni 'Navy' neno la Kiingereza lenye maana ya Jeshi, pili ni 'Kenzo' neno lenye asili ya Japan likiwa na maana ya Busara, Afya na Akili.

Kwa sasa Navy Kenzo wanafanya vizuri na wimbo wao mpya unaokwenda kwa jina la Your Style.

Tayari Navy Kenzo watoa albamu tatu; AIM (Above Inna Minute) (2016), Story Of The African Mob (2020) na Most People Want This (2023), huku akishinda tuzo za muziki Tanzania (TMA), Soundcity MVP, EATV Awards, Hipipo, WatsUp Awards n.k.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live