Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Naumia ninapolinganishwa na mtoto - Dorah

DORA Naumia ninapolinganishwa na mtoto - Dorah

Wed, 20 Jul 2022 Chanzo: Bbc

Wanswekula Zacharia ndio jina halisi la msanii ambaye anajulikana na wengi nchini Tanzania kama Miss Dora .

Mwaka huu ametimiza miaka 27 na kwake yeye anasema kwamba ni muujiza kwamba yuko hai mpaka leo kutokana na kusumbuliwa na ugonjwa wa Seli Mundu ama Sicke cell katika maisha yake ya utotoni , na hadi sasa anaishi na makovu ya ugonjwa huo .

”Nilipoanza kufahamu maisha nilijikuta kwamba sikuwa nakuwa kwa kimo kama watoto wengine , na hadi sasa muonekano wangu unaoneka nina mwili mdogo sana kuliko wanawake wa kawaida wa rika langu , Ila nimekubali jinsi nilivyo na ninajidhatiti kila siku kuyaishi maisha yangu kimamililifu”anasema Dorah .

Dorah ameshiriki michezo mIngi ya tamthilia nchini Tanzania ikiwemo Kapuni na Juakali iliyozidi kumpa umaarufu.

Katika tamthilia ya Juakali, Dorah anasema kwamba alikubali, kuigiza katika nafasi ambayo inagusia maisha yake angalau kwa kiasi fulani ili kudhihirishia ulimwengu mateso aliyopitia, kutengwa na kunyanyapaliwa.

”Kwa kweli sioni shida ikiwa watu wanaweza kujifunza kupitia maisha yangu halisi ,kwani ninaamini kwamba itamuelimisha na kumpa matumaini angalau mtu mmoja ”anasema Dorah.

Dorah alizaliwa huko Singida nchini Tanzania, yeye ni mtoto wa pili kati ya watoto sita .

Mwanadada huyu anasema kwamba wakati anakua maisha hayakuwa mepesi kwa kuwa wazazi wake hawakuwa na uwezo.

Wakati huo tayari alikuwa ameanza kuugua hali ambayo hawakujua kwamba ilikuwa ni ugonjwa wa Seli Mundu (Sickle Cell), ugonjwa ambao huathiri mfumo wa kinga na inakuwa rahisi mtu kuandamwa na magonjwa mbalimbali katika mwili kutokana na kukosa kinga dhabiti ya kujilinda.

Kwa mujibu wa Dorah, historia yake inavitu vingi na pia inahusu watu wengi ambao wamemlea na kumsaidia kufika alipo.

”Nilichukuliwa nikiwa binti wa miaka 8 na mtawa mmoja aliyekuja nyumbani kwetu kututembelea, baada ya kuona hali sio hali, wakaamua kunipeleka katika makazi ya watoto ambako nilianza masomo yangu na pia kuendelea kupewa huduma za matibabu kutokana na hali yangu”, anasema Dorah.

Aliendelea na masomo yake , huku akipewa matibabu , kulingana na msanii huyu alikuwa ameshauriwa na wataalam wa matibabu yake kwamba hali ya ugonjwa huo wa Seli mundu ingekwisha atakapokuwa mtu mzima.

Japo alipata wasamaria wema ambao walitembea naye katika kuhakikisha kwamba amepata matibabu na hali kadhalika amepata masomo anasema kwamba barabara ya kuishi maisha kwa muonekano alionao haikuwa rahisi, hasa kwa kuwa wengi ni wale ambao walimnyanyapaa licha ya miaka kusonga Dorah aliendelea kuwa na muonekano wa ‘kitoto’ na hilo lilimkosesha usingizi kwa miaka mingi.

Mwanamke huyu anasimulia siku zilizojawa na kiza kikuu ambapo baadhi ya watu katika jamii yake na hata watu waliokuwa karibu naye walimpa machungu mengi kwa kutumia muonekano wake kumdhalilisha.

”Hakuna mtu angependa kuwa tofauti na mwingine, sote tunatamani tuwe sawa kwa hivyo inauma kila wakati baadhi ya watu wakinilinganisha na mtoto, inauma sana kwa sababu nina akili za utu uzima na nina haki kama mwanamke mwengine yule ”Dorah alisema.

Ila siku zilivyozidi kwenda akajiunga na chuo kimoja kusomea uanahabari aliamua kupiga moyo konde na kukubali hatma yake kwamba huenda atakua kama wenzake

Seli Mundu ni ugonjwa gani? Msanii huyu pia aligusia maisha yake ya mahusiano hasa ya kimapenzi na anasema kwamba yuko kwenye mahusiano ya kimapenzi ila hataki kuzungumzia zaidi ya hayo.

"Mwisho wa siku mimi ni mwanamke, anachotaka mwanamke mwingine mwenye umbo la kawaida hata mimi natamani, nina haki ya kuwa na mpenzi, kuheshimika, kwa hiyo inauma wakati mtu anatumia maumbile yangu kunidhalilisha na kuniumiza ila mwisho wa siku lazima niishi ”Dorah anasema.

Dalili za Seli Mundu huanza kuonekana mtoto akiwa na umri wa miezi mitano. Dalili huwa tofauti kwa watu tofauti na hubadilika na wakati. Dalili kubwa ni pamoja na upungufu wa damu mwilini. Mgonjwa pia kuwa seli nyekundu chache.

Kwa kawaida seli nyekundu huishi kwa siku 120 kabla ya kuhitaji kubadilishwa. Lakini seli za mgonjwa wa Seli Mundu huishi kwa siku 10 hadi 20, na kuacha pengo la seli nyekundu.

Bila ya kuwa na kiwango kizuri cha seli nyekundu, mwili haupati oksijeni ya kutosha hali ambayo husababisha uchovu wa mwili.

Kuchelewa kukua na pia kuchelewa kubalehe. Chembechembe nyekundu za damu huupa mwili oksijeni na virutubishi muhimu kwa ukuaji. Upungufu wa seli hizo huweza kusababisha ukuaji wa taratibu kwa watoto wadogo na kuchelewesha balehe kwa vijana.

Kupata vipindi vya Maumivu vya kujirudia mara kwa mara ni dalilili kuu ya ugonjwa huu. Maumivu hutokea wakati seli nyekundu za damu zinapoziba mtiririko wa damu kwenye mishipa midogo ndani ya kifua, tumbo na viungo. Maumivu huweza kutokea vile vile ndani ya mifupa. Maumuvu ya kupindukia huhitaji uangalizi hospitalini.

Kuvimba pia mikono na miguu kunakotokana na seli kuziba damu isifike kwenye mikono na migu pamoja na kupata maambukizi pia ya kila wakati, matatizo ya kuona.

Chanzo: Bbc