Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Natumaini Sugu anakwenda kuwa Rais wa Tanzania huko mbeleni – Professor Jay

7840 Sugu Jay Bongo5 Pix Sugu & Prof Jay

Fri, 11 May 2018 Chanzo: bongo5.com

Mbunge wa Mikumi kwa tiketi ya Chadema, Joseph Haule ‘Professor Jay’ amesema kuwa mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ anakwenda kwenye mchakato wa kuwa rais wa Tanzania kutokana na kile alichopitia.



Professor Jay amesema hayo leo May 11, 2018 kabla ya kuanza kuchangia bajeti ya wizara ya viwanda, biashara na uwekezaji kwa mwaka wa fedha 2018/19. Professor Jay amempongeza Sugu kwa kwenda jela na kurudi na kueleza kuwa hicho kinajenga zaidi.

“Natoa pongezi kubwa sana kwa pacha wangu a.k.a Sugu kwa kuhitimu mafunzo huko ndani ambayo yameongeza ujasiri na CV yake ya kisiasa na nanitumaini sasa hivi hatakuwa rais wa Mbeya bali anakwenda katika mchakato wa kuwa Rais wa Tanzania huko mbeleni,” amesema Professor Jay.

Pongezi kama hizo, zimetolewa pia na mbunge wa viti maalum (Chadema), Devotha Minja ambaye amesema kilichompata Sugu ni harakati za ukombozi wa taifa la Tanzania.

Sugu aliachiwa huru hapo jana May 10, 2018 baada kutumikia kifungo kwa zaidi ya miezi minne. Alihukumiwa kifungo cha miezi mitano jela February 26, 2018 kwa kutoa lugha ya fedhea dhidi ya Rais John Magufuli.

Loading...
Chanzo: bongo5.com