Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

"Nasubiri ndoa kwa sasa" - AngelMary Kato

Anweb "Nasubiri ndoa kwa sasa" - AngelMary Kato

Wed, 19 May 2021 Chanzo: eatv.tv

Kama ulikuwa kwenye mipango ya kumpata mtoto AngelMary Kato jua kabisa umegonga mwamba kwani msanii huyo ameweka wazi kwamba yupo kwenye mahusiano na mchumba wake na kinachosubiriwa ni ndoa tu kwa sasa.

Submitted by Shaluwa Anta on Jumanne , 18th Mei , 2021 Msanii AngelMary Kato

Akiweka wazi jambo hilo kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio AngelMary Kato amesema "Kwa upande wa mahusiano mimi nina mchumba wangu tayari na tunachokisubiri kwa sasa ni ndoa".

Kitu kingine alichosema msanii AngelMary Kato ni kucheza filamu moja na staa wa muziki Afrika Awilo Longomba iitwayo 'Life to regret' ambapo ataigiza kama Mke wa Awilo kwenye filamu hiyo.

Kwa sasa AngelMary Kato na Awilo Longomba wamefanya collabo moja inayoitwa Tanzania ambapo inazungumzia kuhusu mazingira ya nchi yetu ya Tanzania.  

Chanzo: eatv.tv