Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

“Nasisitiza hizi ni zama za kazi sio kiki" Hassan Abbasi

MSEMAJI 660x400 1 “Nasisitiza hizi ni zama za kazi sio kiki" Hassan Abbasi

Thu, 18 Feb 2021 Chanzo: millardayo.com

Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Hassan Abbasi, ametoa msimamo kuwa Serikali haitapoteza muda na Wasanii wanaoendeleza kiki badala ya kutumia muda wao vizuri kutengeneza kazi zao bora za sanaa.

Dkt. Abbasi ameyasema hayo Dar es Salaam leo alipokuwa akitembelea eneo la Kivukoni ambapo Serikali inakamilisha taratibu kuziweka katika ofisi moja Taasisi za Sanaa ambazo ni Baraza la Sanaa Tanzania (Basata), Taasisi ya Hakimiliki (Cosota) na Bodi ya Filamu Tanzania (FBT).

“Serikali kama alivyoahidi Rais ipo kazini kuhakikisha Sekta za Sanaa zinakua na kuwapatia Vijana mchango chanya, hapa leo tunapambania Taasisi zetu hizi muhimu kwa Wasanii wapate ofisi nzuri na wahudumiwe kutokea sehemu moja baada ya malalamiko ya miaka mingi kuwa ziko mbalimbali lakini unashangaa baadhi ya Wasanii kuwaona siku mbili hizi wanaturudisha nyuma kwenye maisha ya kiki badala ya kazi bora”- Dkt. Abbasi

Amesema Serikali haitakuwa upande wa Wasanii wanaovunja Sheria za Nchi na taratibu za kimaadili kwa manufaa yao binafsi badala yake itafanya kazi na Wasanii wanaozidi kujielewa na wanaojua sanaa ya Tanzania iko wapi inatakiwa kwenda wapi.

“Jana nimeletewa habari nyingi sana, wengine wamepelekana polisi, wengine unasikia hivi, hawa wanaotaka kuturudisha nyuma Serikali hii haiwezi kuwaendekeza hao, nawapongeza Wasanii wote wawe wa muziki au filamu na sanaa nyingine wanaoendelea kupambana na kutoa kazi bora zinazoendelea kuiheshimisha sanaa yetu”- Dkt. Abbas

“Nasisitiza hizi ni zama za kazi sio kiki, waambieni hao vijana, wafikishieni ujumbe huu, anayesikia na asikie, hii ni sauti na amri kutoka Serikali Ku”- Dkt. Abbasi

Chanzo: millardayo.com