Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nashindana na yeyote sio Rostam pekee – Moni Centrozone

1281 25039150 2020284387987697 4073651303434158080 N TZW

Mon, 15 Jan 2018 Chanzo: bongo5.com

Msanii wa muziki Bongo, Moni Centrozone amesema anashindana na msanii yeyote katika muziki na sio Roma na Stamina (Rostam) kama inavyodaiwa.

Country Boy na Moni (MoCo)

Kauli ya Mone imekuja mara baada ya yeye kuungana na Country Boy na kuanzisha ‘umoja’ wao (MoCo) kitu ambacho kimetafsiriwa kama kushindana na Rostam.

Rapper huyo ameiambia FNL ya EATV kuwa licha ya kutaka kuleta ushindani lakini si Rostam pekee ambao wamekwishafanya kitu kama hicho bali kuna wasanii kama AY na Mwana FA.

“Kwa hiyo kama wameona tupo kwenye ushindani najisikia faraja kuona umefanya kitu na mwanzo wake umeona kipo kwenye ushindani. Nashindana na mtu yeyote ambaye yupo kwenye ushindani wa kimuziki na kibiashara sio Rostam pekee,” amesema Moni.

MoCo kwa sasa wanafanya vizuri na ngoma yao mpya inayokwenda kwa jina la Mwaaah.

Chanzo: bongo5.com