Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Napoleon: Idris Elba kusoma script yako tu unamlipa tsh mil 90

ELBA NAPELONE Idris Elba na Ernest Napeleon

Wed, 12 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Imefahamika kuwa, kufanya kazi na muigizaji maarufu Duniani kutoka nchini Uingereza, Idrissa Akuna Elba (50) ni kazi ngumu kwani jamaa sio mwepesi kama watu wanavyodhani.

Hayo yamethibitishwa na Ernest Napoleon ambaye ameeleza jinsi alivyojaribu kumuingiza Idris Elba kwenye moja ya movie zake.

Napoleon anasema ni ngumu sana kumpata #IdrisElba labda upite kwa wakala wake lakini hata ukifanikiwa kumfikia wakala huyo basi uwe umejipanga kimkwanja.

Napoleon amesema kumpata Idris utachajiwa kiasi cha Paundi 30,000 (zaidi ya tsh milioni 90) kwa ajili ya kusoma script yako tu na hapo huna uhakika kama Idris ataipenda au la!

Napoleon ambaye ni Muigizaji, Mtayarishaji na muandika script wa filamu mbali mbali kama #Kiumeni #Peponi na nyingine nyingi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live