Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Napenda kula, nitapungua nikipata ajira - Love wa Jua Kali

Love JUA Kali Napenda kula, nitapungua nikipata ajira - Love wa Jua Kali

Mon, 19 Feb 2024 Chanzo: Mwananchi

Kwa sasa habari ya mjini kwa baadhi ya wanawake hasa maarufu ni namna wanavyopambana kutengeneza miili yao kwa upasuaji ili kuwa na mionekano ya tofauti.

Hilo lilikuwa likifanyika mataifa makubwa kama China na Uturuki lakini sasa mambo yamebadilika kwani wameletewa karibu zaidi hapa nchini katika Hospitali ya Mloganzila.

Kali ni kwamba wakati wengi wakifanya hivyo staa anayefanya vizuri kwenye tamthilia ya Juakali, Love Pande maarufu kama Love wa Juakali yeye amekiri kuupenda mwili wake na hajawahi kufikiria kuubadilisha.

Hata hivyo Love ameiambia Mwananchi kuwa, atapunguza mwili wake kama kutakuwa na ajira lakini tofauti na hilo atabaki alivyo.

Pamoja na hayo amesema kitu anachopenda zaidi ni kula, japo kuwa kuna muda analazimika kula mara moja kwa siku kutokana na kutingwa na kazi lakini akiwa nyumbani bila lazi huwa anakula zidi ya mara tatu.

"Siyo kula tu mimi hata kwenye suala la kulala nipo vizuri ndiyo starehe yangu ya pili, baada ya kula ukitaka kunikwaza nisumbue wakati wa kulala sipendi usumbufu kabisa linapofika suala hilo," anasema.

Chanzo: Mwananchi