Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nape Nauye ampa neno zito Alikiba

Sfd Nape Alikiba Nape Nauye ampa neno zito Alikiba

Mon, 11 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Moses Nauye amempongeza Msanii wa muziki wa Bongo Flava, Alikiba kwa kufungua kituo chake cha redio cha Crown FM na kusema Serikali itampa leseni na kumsaidia kuweza kuisambaza kote nchini.

Nape alikuwa mgeni rasmi katika sherehe ya miaka 20 ya Aliliba. Hafla hiyo ilifanyika tarehe 09 Machi, 2024 katika ukumbi wa hoteli ya Kilimanjaro (Hyatt Regency Hotel) jijini Dar es Salaam.

"Nimefurahi kuona umefanya uwekezaji ukiwa bado kijana na nguvu, Serikali kupitia Rais Samia itakupa leseni na kukusaidia kuifanya redio yako ifike kote nchini. Sasa ukapambane na usisahau kwenye teknolojia," amesema Nape NNauye.

Hafla hiyo ilihudhuriwa na viongozi mbalimbali, ikiwa ni pamoja na Mgeni Maalum ambaye ni Rais wa Awamu ya Nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais - TAMISEMI, Mohammed Mchengerwa (Mb). Pia, wasanii mbalimbali wa muziki wa kizazi kipya pamoja na wadau wa muziki walikuwepo.

Katika hafla hiyo, Alikiba alitumia fursa hiyo kuzindua redio yake mpya iitwayo Crown FM 92.1. Redio hiyo inapatikana katika maeneo ya Dar es Salaam, Zanzibar, Tanga na Pwani.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live