Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Naomi apata mtoto wa pili akiwa na miaka 53

Naomi Campbell Mtoto.png Naomi apata mtoto wa pili akiwa na miaka 53

Fri, 30 Jun 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Akiwa na miaka 53, Mwanamitindo Naomi Campbell, amefanikiwa kupata mtoto wa pili ambaye ni wa kiume.

Naomi alipata mtoto wake wa kwanza wa kike mwaka 2021, akiwa na miaka 50 ambapo baadhi ya watu walidhani kuwa sio wa kwake, lakini alifafanua hilo kupitia mahojiano maalumu na Jarida la Vogue akisema ni damu yake.

Mrembo huyo ametangaza ujio wa mtoto wake huyo wa pili kupitia ukurasa wake wa Instagram ambapo amewatia moyo wanawake waliokata tamaa ya kupata watoto kutokana na sababu mbalimbali akisema: “...haujachelewa kuwa mama.”

“Kipenzi changu jua kwamba unathaminiwa kupita maelezo na umezungukwa na upendo tangu tu pale taarifa za ujio wako, wewe ni zawadi kutoka kwa Mungu,” ameandika.

Hata hivyo, hadi sasa mrembo huyo hajaweka wazi majina ya watoto wake wala kuonyesha sura zao mitandaoni.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live