Rais wa Shirikisho la Muziki Tanzania, Ado November amezungumza kuhusu sakata la Zuchu na Enock Jonas, amesema kwamba suala hilo limemfikia na jitihada za kutatua jambo hili zinaendelea.
Mbali na hayo Ado amesema kwamba, Enock kumshitaki Zuchu kumefanya wasanii wengine kuja kwake na kushitaki kwamba kuna wasanii wawili wameiga nyimbo yao bila ruhusa yoyote.
Ijapokuwa Ado hajawataja wasanii hao, lakini za ndani kabisa zinaeleza kuwa ni InAfrika band, kwa kuwa ngoma yao "Indege" ndio 'imekopiwa' hivi karibuni na wanamuziki wawili, Nandy na Aggy Baby.
Kutokana na hilo, wadau wanahoji kuwa, kwa mwendo huu mbona wasanii watanyooka, sasa inafrika band wakitaka na wao million 500, Aggy Baby atazitoa wapi?