Supastaa wa Bongo Fleva, Faustina Charles Mfinanga ‘Nandy’ amesema yeye anatamani mtoto wao wanaotarajia kumpata hivi karibu awe wa kike wakati mumewe ambaye pia ni msanii wa Bongo Fleva, William Lyimo ‘Billnass’ akitamani mtoto huyo awe wa kiume.
Nandya ambaye ni mjamzito amesema yuko mwishoni na kwa maana ya mwezi wa mwisho wa ujauzito wake hivyo wakati wowote anaweza kujifungua.
“Huwezi amini tumesema hii iwe sapraizi, sijaenda kutazama kujua iwapo ni wa jinsia ya kiume ama wa kike, lakini naona watu mtandaoni wanasema atakuwa wa kiume, hao wanamfurahisha baba yake. Billnass anatamani sana mtoto wa kwanza awe wa kiume wakati mimi natamani awe wa kike.
“Nina tamani awe wa kike kwa sababu atakuwa rafiki yangu, si kwamba wa kiume hawezi kuwa rafiki yangu, akija wa kiume nitampenda pia. Mtoto wa kike huwa ni mtoto wa baba lakini akiwa wa kike nitasema nimeleta kopi ya kwangu.
Mama yangu huwa ananiambia, 'ka kike hako', nafurahi lakini huwezi kujua maana ya Mungu ni mengi. Kwa hiyo tusubiri,” amesema Nandy.
Aidha, Nandy ambaye ana shoo kesho Jumamosi, Agosti 6, 2022 jijini Mwanza amesema kuwa tamasha lake la Nandy Festival litaendelea kufanyika hata baada ya kujifungua kwakwe kwani si msanii pekee anayefanya shoo bali tamasha hilo linaendeshwa na kampuni yake na wapo wasanii wengi wakubwa wanaopafomu akiwemo Alikiba.