Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nandy kutoa burudani leo tamasha la ZIFF

Sat, 14 Jul 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Usiku wa kuamkia leo Ijumaa Julai 13, 2018, msanii Faustina Charles maarufu Nandy ameshindwa kutumbuiza katika tamasha la filamu za Zanzibar (ZIFF).

Watu wa kada mbalimbali waliofika kushuhudia tamasha hilo la 21 linalofanyika katika viwanja vya Ngome Kongwe visiwani hapa, licha ya kutoshuhudia burudani kutoka kwa Nandy, waliburudika na shoo nzuri kutoka kwa Hellen George maarufu Ruby.

MCL Digital lilizungumza na uongozi wa ZIFF na kubainisha kuwa ratiba ilibadilishwa, hivyo Nandy atatoa burudani leo.

"Ni kweli kutokana na ratiba Nandy na Ruby walipaswa kuimba jana, halafu Aslay na The Mafiki wataimba leo. Ratiba imebadilika na Nandy ataungana kuimba leo na akina Aslay,” amesema Daniel Nyalusi, meneja wa ZIFF.

Watu waliohudhuria tamasha hilo jana walionekana kuwa na shauku ya kupata burudani kutoka kwa Nandy.

 

Chanzo: mwananchi.co.tz