Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nandy kiroho safi akubali kushindanishwa na Zuchu

Zuchu Nandy M.jpeg Nandy kiroho safi akubali kushindanishwa na Zuchu

Sun, 13 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

The African Princess, Faustina Charles Mfinanga 'Nandy' amesema haoni tatizo mashabiki kumshindanisha na mdogo wake kwenye gemu, Zuhura Othuman 'Zuchu'.

Nandy ameyasema hayo usiku wa kuamkia jana Agosti 12, 2023 alipokuwa kwenye usiku wake uliokwenda kwa jina la Follow The Vibe, ambapo alipewa mic na waandishi wa habari ndipo akafunguka.

"Sioni tatizo mimi watu kunishindanisha na Zuchu kwa sababu ni msanii mzuri, ningeona tatizo labda kushindanishwa na msanii labda ambaye si mkubwa au mzuri," alisema Nandy.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live