Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nandy awalipua wanaojadili kichwa cha mwanaye

Ert Nandy Kenaya Nandy awalipua wanaojadili kichwa cha mwanaye

Tue, 29 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baada ya walimwengu kumshambulia mtoto wa masupastaa wa Bongo Fleva, Nandy na Billnas aitwaye Kenaya kuwa hana kichwa kizuri, hatimaye Nandy amefanikiwa kutuliza shobo za Wabongo.

Mange Kimambi ni miongoni mwa watu waliokiri kuwa kichwa cha mtoto huyo akidai kuwa hakina shepu hivyo amemshauri akipata mtoto wakati mwingine anunue helmet amvalishe mtoto siku za mwanzoni kabla mifupa haijakomaa ili kichwa kiwe na muonekano mzuri, kwani mastaa wengi wa Ulaya wanafanya hivyo kwa watoto wao.

nandya ameibuka na kujibu; "Hatuyumbishwi na maneno ya mtandaoni kwa sababu tulijiandaa, kabla hatujamuanika mtoto wetu tulijipanga kukabiliana na kila litakalotokea.

"Kwa sababu tulikuwa tunaona kwa watoto wa mastaa wengine wanavyoatakiwa, lakini mtoto wetu ni mtoto kama walivyo watoto wengine tungeomba aheshimiwe.

"Kabla hatujampa jina la Kenaya tulichagua majina mengi tukayapigia kura tukapata jina hilo kwa sababu pia tuliona lina maana nzuri, Kenaya maana yake ni (Glory to God)," amesema Nandy.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live