Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nandy atoa kauli ya kibabe ndoa yake na Billnass

Nandy Billnass Nandy na Billnass

Thu, 14 Apr 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

MWIMBAJI wa Ngoma ya Siwezi, Nandy ameweka wazi kuwa yeye atakuwa msanii wa mfano Tanzania ambaye atawaaminisha watu tofauti pindi watakapofunga ndoa na rapa Bill Nass.

Nandy alisema watu wanaamini kuwa msanii wa kiume au wakike akioa au kuolewa, inakuwa ndiyo sababu ya kushuka kimuziki, yeye atakuwa msanii wa kwanza mwanamke atakayeolewa na kubaki kuwa juu.

Nandy alisema: “Kumekuwa na hayo maneno sana mtaani ya kuwa kama mwanamke ukiolewa unashuka kimuziki, ingawa kuna ukweli ndani yake, mimi nitaionyesha dunia kuwa unaweza kuolewa na kubaki kuwa juu kimuziki.”

Nandy yupo mbioni kufunga ndoa na mchumba wake Bill Nass, baada ya kuvishana pete miezi kadhaa iliyopita.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live