Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nandy atangaza hali ya hatari 'nitawasuuza mioyo'

Nandy Kusuuza Mashabiki Nandy atangaza hali ya hatari 'nitawasuuza mioyo'

Fri, 4 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

The African Princess Faustina Charles Mfinanga 'Nandy' amestangaza kuwa soon atadondosha ngoma mpya ambayo itakuwa balaa.

Nandy ameweka ujumbe huo kupitia Insta Story yake ambapo amesema, wimbo huo wa kuchezeka, utakuwa wa kila mtu kuanzia mtoto, kijana na hata mtu mzima.

"Ni wimbo ambao kila mtu ataimba, hatubagui mtoto, mkubwa, mzee wote wata bang nao. Nimemaliza kikao cha tarehe ya kutoka, soon nakuja wajuza mashabiki zangu comment na DM zenu naziona, nakuja kuwasuuza mioyo," alisema Nandy.

Nandy atakapoingiza ngoma mpya sokoni, atakwenda kuchuana na Enjoy ya Jux ya Diamond pamoja na Honey ya Zuchu ambayo inakamata nafasi ya kwanza trending kwa sasa huko mjini YouTube.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live