Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nandy ashangazwa na kauli hii ya Ruby

Mon, 29 Jan 2018 Chanzo: bongo5.com

Msanii wa muziki Bongo, Nandy amejibu kauli ya Ruby ambayo ilidai alikaa kimya kimuziki kumpisha muimbaji huyo kufanya vizuri.



Nandy amesema hilo halina ukweli wowote kwani tangu alipoondoka katika uongozi wake kuna nyimbo ambazo alitoa, hivyo kutoa kauli kama hiyo ni kujitetea.

“Sio kweli kwa sababu nakumbuka ana nyimbo tatu kazitoa kipindi ambacho amesema amepumzika, katoa singeli mbili na wimbo mmoja unaitwa Wale Wale, sasa hapo alikuwa amepumzika au ni kitu ambacho si cha kweli,” amesema.

“Halafu watu walikuwa wanajua amegombana na uongozi wake ndio akatoa hizo nyimbo ni kisingizio cha kujitetea,” Nandy ameiambia EATV.

Kwa sasa Nandy anafanya vizuri na wimbo ‘Subal kheir’ alioshirikiana na Aslay ambao awali uliimbwa na Culture Group kutoka visiwani Zanzibar.

Chanzo: bongo5.com