Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nandy amtaja mumewe kufungua mgahawa

Nandy Kiwanja Nandy amtaja mumewe kufungua mgahawa

Tue, 8 Nov 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mungu anazidi kumfungulia njia mtoto mzuri ndani ya Bongo Fleva, Faustina Charles Mfinanga ‘Nandy’ ambapo safari hii, amefungua mgahawa wake maeneo ya Goba jijini Dar.

Akizungumza kwenye uzinduzi huo alioufanya juzikati, Nandy alisema kufungua biashara hiyo ilikuwa ni ndoto yake kabla hajatimiza miaka thelathini hivyo anamshukuru Mungu kwa kutimiza ndoto hiyo.

“Mume wangu amenisaidia sana mawazo maana ilikuwa ni ndoto yangu lakini pia menejimenti yangu imenisaidia kwa kiasi kikubwa,” alisema Nandy.

Mgahawa huo ameupa jina la NON akimaanisha Nandy au Nandera huku akisema tajitahidi kuboresha kila siku na amaamini hauwezi kufa kama kwa baadhi ya wasanii waliowahi kuanzisha biashara hiyo kisha ikawashinda.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live