Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nandy alivyopiga mwereka akishuti Bye

Kava Nandy Na Bill Nandy alivyopiga mwereka akishuti Bye

Sat, 23 Jul 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Bibi harusi mpya mjini, Faustina Charles Mfinanga 'Nandy' ameshea na mashabiki wake moja ya kipande cha video kikimuonesha akiaanguka chini wakati anarekodi video ya wimbo wa mumewe Billnass, Bye.

Kwenye kipande hicho cha video Nandy anaonekana akiwa anatembea kwenye korido akiwa amevalia gauni refu ambalo lilimfanya aanguke baada ya kulikanyaka na kukosa balansi akajikuta ameanguka mzimamzima puuu!

"Yaani Hanscana ulitaka mpaka hii video inaisha umenivunja mguu? Umeona nilivyopata shida lakini! Sema Billnass kachupa kaukumbusho kamenyooka na hili goma lazima liimbwe leo Songea," ameandika Nandy chini ya kipande hicho cha video.

Nandy anatarajia kukamua shoo yake ya ufunguzi wa Nandy Festival leo pande za Songea.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live