Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nandy ajibu ishu ya ushirikina unaodaiwa kufanywa na Lulu Diva

Nnady Na Lulu Diva Nandy ajibu ishu ya ushirikina unaodaiwa kufanywa na Lulu Diva

Wed, 6 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Hatimaye msanii Nandy amevunja kimya chake baada ya sauti kuvuja ikikisiwa kuwa ya msanii mwenza wa kike akizungumza na mganga kuhusu mafanikio yake kimuziki.

Jumatano mitandao ya kijamii huko nchini Tanzania ilisisima baaada ya sauti inayodaiwa kuwa ya msanii Lulu Diva akizungumza na mtaalamu wa uganga kuhusu mafanikio yake kimuziki.

Katika sauti hiyo, anayedaiwa kuwa ni Diva alisikika akimwambia Mganga kufanya makeke ilia pate kuwa msanii wa pekee wa kike nchini Tanzania anayependwa Zaidi na mashabiki, akidai kwamba anataka nyota yake ing’ae Zaidi kuliko ile ya Nandy.

Pia alimshukuru mganga huyo kwa kile alisema alifanya jambo zito lililofanya ngoma yake ya ‘Andazi’ kufanya vizuri na kupokelewa hadi vijijini, hivyo akamtaka kumfanya apate umaarufu na shoo kibao kila uchao kama anavyopata Nandy.

“Kwenye Andazi tumekwisha, yaani kama ni ile kafara tumefanya basi tumetisha na tumeua kwa sababu ile Andazi imeenda vizuri yaani mpaka kule vijijini nikienda ninaisikia, watu wanaitika. Lakini sasa mtaalamu nashangaa mbona shoo sipati, huu mwisho wa mwaka mbona simu haziiti? Naishia tu kuona wasichana wengine wakifanya shoo, mbona sipati hizo shoo mimi? Mimi ninachotaka nipate hizo shoo hivyo,” alisema kwa sehemu.

Sasa baada ya kutaja baadhi ya mafanikio ya Nandy na kusema angependa awe kama yeye kupata shoo nyingi kila wikendi, Nandy amekwenda kwenye mitandao ya kijamii na kujibu akisema kwamba anakemea pepo hilo.

Nandy alipakia picha akiwa ameweka noti za dola kwenye miwani machoni na kuandika kwamba anakemea kila pepo inayotamani mafanikio yake.

“Leo na kemeaa ma pepo…. Ya kutamani tamani maisha yangu!!” Nandy aliandika.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live