Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nandy aja ‘kivingine’ na EP ya Nyimbo za Dini

WhatsApp Image 2021 02 11 At 13.42.05 660x400.jpeg Nandy aja ‘kivingine’ na EP ya Nyimbo za Dini

Mon, 8 Mar 2021 Chanzo: millardayo.com

Hatimaye nyota wa muziki nchini Tanzania, The African Princes ‘Nandy’ ameachia EP yake Nyimbo za Dini ‘Wanibariki’. EP hiyo ina nyimbo tano ambazo ni ‘Wanibariki’, ‘Umenifaa’, ‘Nipo Naye’, ‘Asante’ na ‘Noel Song’.

Nandy, jina halisi, Faustina Charles Mfinanga amesema alikuwa na ndoto ya kutoa kazi yenye Nyimbo za Dini siku moja kwa sababu amekuwa mpenzi mkubwa wa nyimbo hizo tangu akiwa mtoto hivyo, kwa kufanikiwa kuachia EP hii ya ‘Wanibariki’ ametimiza ndoto zake.

“Tangu nikiwa mdogo nimekuwa sana nikimpenda sana Mungu, mimi ni muumini mzuri sana wa kanisani na kitendo cha kutoa EP hii (Wanibariki), nimetimiza ndoto zangu,” Nandy.

‘Wanibariki EP’ imetayarishwa kwenye studio za Wanene kwa ushirikiano wa karibu na kampuni ya Boomplay na Nandy mwenyewe.

Mbali na EP hii, Nandy amewahi kufanya ‘cover’ za nyimbo za dini za waimbaji kama Joel Lwaga (Mimi Ni Wa Juu) pamoja na Angel Benard (Nikumbushe Wema Wako).

Chanzo: millardayo.com