Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nandy aikacha fungate, apiga kazi na kitumbo chake

Nandy Na Billnass Church Nandy aikacha fungate, apiga kazi na kitumbo chake

Wed, 20 Jul 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mchana huu Jumatano Julai 20, 2022, bibi harusi, Nandy au Nandera, kabla hata ya siku saba baada ya ndoa na Billnass ameonekana hadharani na kuzua maswali.

Nandy alikuwa anasaini dili la ubalozi wa bima ya afya ya kwake na mtoto anayetarajia kujifungua soon.

Wakati akishukuru kwa dili hilo Nandy anasema; “Watu wanashangaa, lakini naomba niwatoe tena wasiwasi kuwa mjamzito siyo mtu wa kukaa ndani.”

Anasema atashiriki tamasha lake la Nandy Festival mjini Songea bila wasiwasi wowote kwani kila kitu amewekewa vizuri kuanzia sasa hadi atakapojifungua na kulea mtoto wake yeye na mumewe, Nenga.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live