Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nandy afurahia ubalozi wa Flowless

Da4d6e789118b3f83d12faa19fe5abfe Nandy afurahia ubalozi wa Flowless

Fri, 12 Feb 2021 Chanzo: habarileo.co.tz

MSANII wa muziki wa kizazi kipya, Faustina Mfinanga ‘Nandy’ ametangazwa kuwa balozi wa taasisi isiyokuwa ya kiserikali ya T-Marc kupitia taulo zake za kike za Flowless.

Akizungumzia ubalozi huo, Nandy alisema kunatokana na matunda ya kazi nzuri ya kuburudisha jamii kwa njia ya sanaa na imani waliyonayo kampuni ya T-Marc kutokana uwezo wake wa kufikisha ujumbe wa hedhi salama kwa jamii ndiyo maana amepewa fursa hiyo.

Alisema kupitia nyimbo zake amekuwa akifundisha, kuelimisha na kuburudisha jamii juu ya mambo mbalimbali na kwamba kupitia ubalozi huo atahakikisha wanawake wanalinda afya zao kipindi cha hedhi kwa kutumia taulo za Flowless.

“Ninazijua taulo za Flowless ni kwa ajili ya wanawake wenye ndoto kubwa, wanaojiamini na kuwa tayari kupambana kufikia malengo ya maisha yao siku zote,” alisema.

Mkurugenzi wa biashara na jamii wa taasisi hiyo, Flavian Ngole alisema msanii huyo ana mchango mkubwa katika jamii hususan kwenye kuelimisha, kujiamini, kujituma kwenye kazi kwa malengo na ana ushawishi mkubwa kwa vijana wa kike ndani na nje ya nchi.

Alisema lengo ni kufikisha ujumbe kwa wanawake wote wa ndani ya nje ya nchi kuhusiana na umuhimu wa kutumia pedi hizo na taasisi imeona ni vema kumtumia Nandy ili awafikishie ujumbe huo wanawake wote.

“Taasisi inatambua nafasi ya sanaa katika jamii, inaweza kufanya kazi kubwa kwa jamii na ndiyo maana tunawatumia wasanii wa hapa nchini kwenye bidhaa zetu ndio maana tumemtumia Nandy kutangaza bidhaa hii ya pedi za Flowless” alisema Ngole.

Chanzo: habarileo.co.tz