Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nandy adaiwa kujifungua

NANDY BILLNASS PUNDAZ Nandy adaiwa kujifungua

Mon, 22 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Nandy; ni malkia wa Bongo Fleva ambaye ndoa yake na rapa Billnass inadaiwa kujibu baada ya kujifungua mtoto wa kike (sistaduu) kimyakimya.

Diva The Bawse ni mtangazaji wa Wasafi ambaye kupitia kurasa zake za kijamii amethibitisha hilo mara tu baada ya Tamasha la Nandy Festival kusitishwa hadi mwakani.

Waandaaji wa Tamasha la Nandy Festival 2022 wametangaza kuahirisha tamasha hilo kutokana na hali ya kiafya ya Nandy (mzazi) ambaye ni mwanzilishi wa tamasha hilo.

Taarifa ya kuahirishwa kwa tamasha hilo ilieleza kuwa, walitarajia kufanya tamasha hilo kwenye mikoa mitano nchini Tanzania, lakini wameishia kwenye mikoa miwili ya Mtwara na Mwanza ambapo Arusha ndiyo ilikuwa inafuata.

Nandy na Billnass wameendelea kupokea hongera kama zote kutoka kwa marafiki, ndugu na baadhi ya wasanii wenzao ambapo wenyewe hawajasema chochote kuhusu ugeni huo kwenye familia yao.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live