Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nandy, Zuchu kimenuka! Mwijaku avushisha audio yenye tuhuma nzito

Zuchu Nandy M.jpeg Nandy, Zuchu kimenuka! Mwijaku avushisha audio yenye tuhuma nzito

Fri, 22 Jul 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Msanii wa Bongo Fleva, Nandy ameonekana kukanusha taarifa ambazo msanii mwenzake wa kike Zuchu alisema alipata dili la kutangaza kinywaji cha pombe lakini akalikataa.

Zuchu alisema alikataa dili hilo kwa sababu ya Imani yake ya Kiislamu ambayo haimruhusu kujihusisha na masuala ya pombe, hivyo dili hilo akapewa msanii mwenzake Nandy ambalo alisaini hivi karibuni.

Katika audio iliyosambaa mitandaoni, anasikika Zuchu akimpa maelekezo Mwijaku aisambaze taarifa hiyo akisema dili hilo amelipambania kwa jasho na kulipa kwa sababu ni msanii mkubwa kuliko Zuchu, hivyo vigezo vyake ndivyo vimemfanya akapewa dili hilo nono wala si kwamba lilikuwa dili la Zuchu kama anavyodai.

“Mwijaku, hapo ambapo inasema walikuwa wasanii wangapi akiwemo Zuchu, itoe hiyo point, andika hivi ‘hakuna mtu ambaye atapewa dili la hela nyingi alikatae, especially la pombe’, kwa sababu watahisi tumesema zaidi, tumeongea details za ndani,” amesikika sauti ya Nandy kwenye sehemu ya audio hiyo akizungumza.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live