Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nandy: Tumeanza Vikao

Nandy Pete Nandy: Tumeanza Vikao

Thu, 3 Feb 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

MALKIA wa Bongo Fleva, Nandy The African Princess anasema kwamba vikao vimeanza kwa ajili ya maandalizi ya tamasha lake la Nandy Festival 2022.

Nandy anasema kwamba, vikao vya kupanga mikakati ya tamasha hilo mwaka huu wa 2022 tayari vimeanza huku akiwaomba mashabiki kumpa sapoti kwa ajili ya shughuli hiyo.

“Kikao cha kwanza cha leo cha mwaka huu cha Nandy Festival 2022. Mshindwe nyie mashabiki…” anasema Nandy au Nandera; jina la utotoni.

Mwaka jana, tamasha hilo lilifanyika katika mikoa mbalimbali huku mashabiki wakijitokeza kwa wingi kushuhudia burudani kutoka kwa wasanii waliopata nafasi kuingia jukwaani.

Kinachosubiriwa ni kuona utofautigani ambao Nandy ataleta katika tamasha hilo kuanzia kwa muundo wa jukwaa, wasanii na hata mbinu yake ya kufanya mauzo ya tamasha hilo.

Kwingineko, baadhi ya mashabiki wanazidi kushangaa kama Nandy ataweza kurudia miondoko yake ya dansi aliyotumia mwaka jana ikifahamika kwamba mwanadada huyo ameongeza uzani si haba.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live