Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nandy: Siwapendi marafiki wa Billnass

Nandy Na Billnass Church Nandy: Siwapendi marafiki wa Billnass

Fri, 5 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Msanii wa Bongo Fleva, Faustina Mfinanga ‘nandy’ amefunguka kuwa katika kipindi hiki cha ujauzito wake anawachukia marafiki wa mumewe, Billnass kuliko kawaida mpaka wao wenyewe wananishangaa.

Nandy amesema hali hiyo imemtokea katika kipindi cha ujauzito lakini anaamini atakuwa sawa baada ya kujifungua hasa marafiki wa Billnass anaofanya nao biashara pamoja na si wasanii wenzake.

“Tangu nimekuwa mjamzito sipendi kabisa marafiki wa mume wangu, sometimes wananiambia ‘mimba yako haitupendi’. Yaani hata wakipiga simu naweza kuipokea mimi…. Imetokea tu kutokelewana na marafiki wa mume wangu.

“Anaweza akanipigia akasema nipo na mtu flani labda ni rafiki yake, kama nina namba yake huyo mtu, nampigia namwambia naomba mume wangu asichelewe, akichelewa najua ni wewe, nakuwa nazingua kabisa. Lakini wakati mwingine najishtukia nasema huyu ni mwanaume, kuna vitu vyake lazima afanye.

“Kipindi cha nyuma nilikuwa nalia hata bila sababu, akinikalipia hata kitu kidogo naona kama nimeonewa, kiasi kwamba nalia hata siku mbili bila kula, mpaka yeye mwenyewe anibembeleze, hakujua kwamba sababu ni mimba mpaka alipoenda kuuliza akaambiwa hiyo ni mimba. Kwa hiyo naye alikuwa ananua nikikasirika.

“Kingine kuna pafyumu nilimnunulia Nigeria akaipenda lakini mimi imetokea tu ninaichukia sana ile pafyumu mpaka yeye mwenyewe ananishangaa, akijipulizia mimi najiskia vibaya inabidi avue shati aweke kwenye nguo chafu avae jingine ndipo aondoke.

“Mimi namwamsha Billnass saa tisa usiku akanitafutie chipsi za Dubai kwa sababu ya njaa. Ninakuwa nimekula chakula changu mapema kawaida, lakini baada ya saa mbili napata njaa naagiza chipsi, ikifika saa 9 usku kama sijalala, njaa tena, namwamsha akanitafutie chipsi ama tunaenda wote, kwa kweli namsumbua mpaka anasema namuonea,” amesema Nandy.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live